Page 14 - Fasihi ya Kiswahili kwa Shule za Sekondari Kiongozi cha Mwalimu Kidato cha Tano
P. 14

Fasihi ya Kiswahili  Shule za Sekondari


           Shughuli ya 2.2

           Hatua za ufundishaji

             (i)   Waongoze wanafunzi kutumia vyanzo mbalimbali vya maarifa
           FOR ONLINE READING ONLY
                  kusoma matini  zinazohusu  shughuli ya 2.2 iliyomo  kwenye
                  Kitabu cha Mwanafunzi.
             (ii)  Waelekeze wanafunzi kukaa katika jozi au vikundi ili kujadili
                  shughuli ya 2.2 iliyomo  kwenye Kitabu cha Mwanafunzi.
                  Katika majadiliano, kila mwanafunzi ashiriki kikamilifu kwa
                  kutoa mawazo juu ya alichokisoma katika matini.

             (iii)  Waongoze wanafunzi kufanya uwasilishaji. Chagua wanafunzi
                  wachache  kuwasilisha  kazi  zao  kwa  niaba  ya  wengine.
                  Hakikisha kila mwanafunzi anashiriki kwa kuchangia mawazo
                  na au kuuliza  maswali  ili  kuboresha kazi  zilizowasilishwa.
                  Rekebisha upungufu unaojitokeza  wakati wa uwasilishaji ili
                  kuleta uelewa wa pamoja.

           Majibu

           Majibu ya shughuli ya 2.2 yatatokana na uelewa wa mwanafunzi. Katika
           shughuli hii, mwanafunzi afafanue kwa mifano utanzu wa hadithi na
           vipera vyake. Majibu yaeleze utanzu wa hadithi na uhusiano wa vipera
           vyake kama vile ngano, vigano, tahiri, soga na visasili.

           Shughuli ya 2.3

           Hatua za ufundishaji

             (i)   Waongoze wanafunzi kutumia vyanzo vya mtandaoni au
                  maktabani kusoma matini mbalimbali zinazohusu shughuli ya
                  2.3 iliyomo kwenye Kitabu cha Mwanafunzi.

             (ii)  Waelekeze  wanafunzi  kukaa  katika  jozi  na  kujadili  shughuli
                  ya 2.3 iliyomo  kwenye Kitabu cha Mwanafunzi. Hakikisha




              8                                        Kiongozi cha Mwalimu
                                                          Kidato cha Tano



                                                                            23/06/2024   17:48
     FASIHI YA KISWAHILI KIONGOZI  CHA MWALIMU KIDATO CHA TANO.indd   8
     FASIHI YA KISWAHILI KIONGOZI  CHA MWALIMU KIDATO CHA TANO.indd   8     23/06/2024   17:48
   9   10   11   12   13   14   15   16   17   18   19