Page 17 - Fasihi ya Kiswahili kwa Shule za Sekondari Kiongozi cha Mwalimu Kidato cha Tano
P. 17
Fasihi ya Kiswahili Shule za Sekondari
Shughuli ya 2.7
Hatua za ufundishaji
(i) Waongoze wanafunzi kutumia vyanzo mbalimbali kukusanya
FOR ONLINE READING ONLY
michezo mitatu ya watoto katika shughuli ya 2.7 iliyomo
kwenye Kitabu cha Mwanafunzi, kisha bainisha mbinu za
kisanaa zilizotumika katika utunzi wa michezo hiyo. Hakikisha
kila mwanafunzi anashiriki kikamilifu huku akichukua nukuu.
(ii) Waongoze wanafunzi kukusanya kazi zao ili kurekebisha na
kuondoa dosari zinazojitokeza, kisha hitimisha kwa kutoa
mrejesho wa shughuli hiyo.
Majibu
Majibu ya shughuli ya 2.7 yatatokana na uelewa wa mwanafunzi. Katika
shughuli hii, mwanafunzi abainishe mbinu mbalimbali za kisanaa
zilizotumika katika kutunga michezo aliyoichagua.
(iii) Waelekeze wanafunzi kufanya zoezi la 2.1 lililomo kwenye
Kitabu cha Mwanafunzi.
Majibu
Majibu ya zoezi la 2.1 yatatokana na uelewa wa mwanafunzi kuhusiana
na maswali hayo. Mwanafunzi atumie mifano dhahiri kutetea hoja kwa
kila swali.
Shughuli ya 2.8
Hatua za ufundishaji
(i) Waongoze wanafunzi kutumia vyanzo vya mtandaoni au
vinginevyo kufanya shughuli ya 2.8 iliyomo kwenye Kitabu
cha Mwanafunzi, kisha kila mwanafunzi akusanye kazi yake
kwa ajili ya kusahihisha na kuondoa dosari zitakazojitokeza.
Kiongozi cha Mwalimu 11
Kidato cha Tano
23/06/2024 17:48
FASIHI YA KISWAHILI KIONGOZI CHA MWALIMU KIDATO CHA TANO.indd 11 23/06/2024 17:48
FASIHI YA KISWAHILI KIONGOZI CHA MWALIMU KIDATO CHA TANO.indd 11