Page 8 - Fasihi ya Kiswahili kwa Shule za Sekondari Kiongozi cha Mwalimu Kidato cha Tano
P. 8
Fasihi ya Kiswahili Shule za Sekondari
kwenye Kitabu cha Mwanafunzi, kisha wakae katika jozi na
washirikishane yale waliyotafakari.
(ii) Wanafunzi wabungue bongo kuhusu dhana ya fasihi kulingana
na wataalamu mbalimbali ili kupata maarifa yao ya awali.
FOR ONLINE READING ONLY
(iii) Waelekeze wanafunzi kukaa katika vikundi au jozi au njia
nyingine unayoona inafaa kulingana na mazingira yako na
kujadili shughuli ya 1.1 na 1.2 zilizomo kwenye Kitabu
cha Mwanafunzi. Hakikisha kila mwanafunzi anashiriki
katika mjadala. Rekebisha dosari zinazojitokeza wakati wa
majadiliano.
(iv) Waelekeze wanafunzi kuandaa uwasilishaji. Chagua wanafunzi
wachache kuwakilisha wengine. Katika uwasilishaji, hakikisha
kila mwanafunzi anashiriki kwa kutoa mawazo yake au
kuuliza maswali. Rekebisha upungufu unaojitokeza wakati wa
uwasilishaji.
Majibu
Majibu ya shughuli ya 1.1 na 1.2 yatatokana na uelewa wa mwanafunzi.
Katika shughuli ya 1.1, mwanafunzi abainishe matini za kifasihi
kulingana na ufahamu na uzoefu wake. Katika shughuli ya 1.2
mwanafunzi atoe maoni kuhusu dhana ya fasihi kwa mujibu wa ufahamu
wake na vyanzo alivyovirejelea.
Shughuli ya 1.3
Hatua za ufundishaji
(i) Waongoze wanafunzi kukaa katika vikundi na kuchambua matini
mbalimbali zinazohusiana na shughuli ya 1.3 iliyomo kwenye
Kitabu cha Mwanafunzi. Kisha, toa nafasi ya kila kikundi
kuwasilisha mitazamo hiyo darasani kwa ajili ya majadiliano
2 Kiongozi cha Mwalimu
Kidato cha Tano
23/06/2024 17:48
FASIHI YA KISWAHILI KIONGOZI CHA MWALIMU KIDATO CHA TANO.indd 2
FASIHI YA KISWAHILI KIONGOZI CHA MWALIMU KIDATO CHA TANO.indd 2 23/06/2024 17:48