Page 28 - Fasihi ya Kiswahili kwa Shule za Sekondari Kiongozi cha Mwalimu Kidato cha Tano
P. 28
Fasihi ya Kiswahili Shule za Sekondari
Somo la 2: Uhusiano wa fani na maudhui katika kazi za fasihi
Shughuli ya 3.2(a)
FOR ONLINE READING ONLY
Hatua za ufundishaji
(i) Waongoze wanafunzi kusoma hadithi teule mojawapo, kisha
wakae katika jozi wajadili shughuli ya 3.2(a) iliyomo kwenye
Kitabu cha Mwanafunzi, hakikisha kila mwanafunzi anashiriki
kikamilifu huku akiandika tini.
(ii) Waongoze wanafunzi kuhitimisha kwa kutoa maelezo ya jumla
yanayohusiana na shughuli husika.
Majibu
Majibu ya shughuli ya 3.2 (a) yatatokana na uelewa wa mwanafunzi.
Katika shughuli hii, mwanafunzi achambue vipengele vya fani na
maudhui katika hadithi teule atakayoichagua kwa kuongozwa na
maswali (i) - (iv). Pia mwanafunzi aoneshe uhusiano wa fani na maudhui
katika kazi yoyote ya fasihi.
Shughuli ya 3.2 (b)
Hatua za ufundishaji
(i) Waongoze wanafunzi kusikiliza au kusoma kazi yoyote ya fasihi
kisha kukaa katika jozi ili kuchambua uhusiano wa vipengele
vya fani na maudhui katika kazi hiyo.
(ii) Waelekeze wanafunzi kubadilishana kazi zao na kila jozi
isome kazi ya wenzao kisha kukosoa dosari watakazozibaini na
kurudisha tena kwa wahusika.
(iii) Waongoze wanafunzi kuuliza maswali yatakayochochea
mjadala na kila mwanafunzi ashiriki kujibu maswali. Rekebisha
upungufu unaojitokeza
22 Kiongozi cha Mwalimu
Kidato cha Tano
23/06/2024 17:48
FASIHI YA KISWAHILI KIONGOZI CHA MWALIMU KIDATO CHA TANO.indd 22
FASIHI YA KISWAHILI KIONGOZI CHA MWALIMU KIDATO CHA TANO.indd 22 23/06/2024 17:48