Page 43 - Fasihi ya Kiswahili kwa Shule za Sekondari Kiongozi cha Mwalimu Kidato cha Tano
P. 43

Fasihi ya Kiswahili  Shule za Sekondari


             (iii)  Waongoze  wanafunzi  kuwasilisha  maadili  yaliyomo katika
                  mashairi,  chagua vikundi  vichache  ili  uwasilishe  kazi  zao,
                  hakikisha kila mwanafunzi anashiriki kikamilifu kisha kusanya
                  kazi za wanafunzi.
           FOR ONLINE READING ONLY
             (iv)  Sahihisha kazi ya kila mwanafunzi ili kuondoa dosari
                  zinazojitokeza na toa mrejesho kwa wanafunzi wote.

           Majibu
           Majibu ya shughuli ya 4.3 (b) yatatokana na uelewa wa mwanafunzi.
           Katika shughuli hii, mwanafunzi atachambua maadili yaliyomo katika
           mashairi kutoka katika diwani teule.

           Shughuli ya 4.4(a)

           Hatua za ufundishaji

             (i)   Waongoze wanafunzi kusoma matini fupi ya tamthiliya iliyomo
                  katika shughuli ya 4.4 (a) katika Kitabu cha Mwanafunzi.
             (ii)  Kwa njia ya maswali na majibu, waongoze wanafunzi kujibu
                  maswali yaliyopo baada ya matini fupi ya tamthiliya.

             (iii)  Waelekeze  wanafunzi  kuchambua  maadili  kisha kukusanya
                  kazi  zao. Sahihisha  na toa mrejesho  wa shughuli hiyo kwa
                  wanafunzi wote.

           Majibu

           Majibu ya shughuli ya 4.4 (a) yatatokana na uelewa wa mwanafunzi.
           Katika shughuli hii, mwanafunzi atachambua maadili kwa kuongozwa
           na maswali yaliyomo katika Kitabu cha Mwanafunzi.


           Shughuli ya 4.4(b)
           Hatua za ufundishaji


             (i)   Waongoze wanafunzi kufanya shughuli ya 4.4 (b) iliyomo
                  kwenye Kitabu cha Mwanafunzi.


                 Kiongozi cha Mwalimu                                    37
                    Kidato cha Tano



                                                                            23/06/2024   17:48
     FASIHI YA KISWAHILI KIONGOZI  CHA MWALIMU KIDATO CHA TANO.indd   37    23/06/2024   17:48
     FASIHI YA KISWAHILI KIONGOZI  CHA MWALIMU KIDATO CHA TANO.indd   37
   38   39   40   41   42   43   44   45   46   47   48