Page 48 - Fasihi ya Kiswahili kwa Shule za Sekondari Kiongozi cha Mwalimu Kidato cha Tano
P. 48
Fasihi ya Kiswahili Shule za Sekondari
wenzao huku wengine wakichangia hoja na kuuliza maswali ili
kuendeleza majadiliano zaidi. Rekebisha upungufu unaojitokeza
wakati wa uwasilishaji.
(iii) Hitimisha kwa kutoa maelezo ya jumla kuhusiana na shughuli
FOR ONLINE READING ONLY
husika.
Majibu
Majibu ya shughuli ya 4.8 (a) yatatokana na uelewa wa mwanafunzi.
Katika shughuli hii, mwanafunzi atatakiwa kulinganisha maadili na
masuala ya kiimani yaliyomo katika kipande hicho cha tamthiliya kwa
kujibu maswali i - v.
Shughuli ya 4.8(b)
Hatua za ufundishaji
(i) Waongoze wanafunzi kufanya shughuli ya 4.8 (b) iliyomo
kwenye Kitabu cha Mwanafunzi.
(ii) Waongoze wanafunzi kuchambua maadili yaliyomo katika
tamthiliya teule mbili, kisha waandae matini ya uchambuzi na
kuikusanya kwa ajili ya maboresho.
(iii) Sahihisha kazi ya kila mwanafunzi ili kuondoa dosari
zinazojitokeza na toa mrejesho kwa wanafunzi wote.
Majibu
Majibu ya shughuli ya 4.8 (b) yatatokana na uelewa wa mwanafunzi.
Katika shughuli hii, mwanafunzi atachambua na kuhusianisha maadili
yaliyomo na imani za jamii katika tamthiliya teule mbili.
42 Kiongozi cha Mwalimu
Kidato cha Tano
23/06/2024 17:48
FASIHI YA KISWAHILI KIONGOZI CHA MWALIMU KIDATO CHA TANO.indd 42
FASIHI YA KISWAHILI KIONGOZI CHA MWALIMU KIDATO CHA TANO.indd 42 23/06/2024 17:48