Page 50 - Fasihi ya Kiswahili kwa Shule za Sekondari Kiongozi cha Mwalimu Kidato cha Tano
P. 50
Fasihi ya Kiswahili Shule za Sekondari
inayopatikana katika nyimbo hizo, huku mwanafunzi akichukua
nukuu.
(ii) Waongoze wanafunzi kukusanya kazi zao. Sahihisha kazi ya
kila mwanafunzi na toa mrejesho kwa wanafunzi wote.
FOR ONLINE READING ONLY
Majibu
Majibu ya shughuli ya 4.9 (b) yatatokana na uelewa wa mwanafunzi.
Katika shughuli hii, mwanafunzi atachambua mitazamo inayopatikana
katika nyimbo alizozichambua.
Shughuli ya 4.10(a)
Hatua za ufundishaji
(i) Waongoze wanafunzi kusoma au kughani shairi la shughuli ya
4.10 (a) lililomo kwenye Kitabu cha Mwanafunzi, kisha kukaa
katika jozi ili kuchambua mitazamo iliyomo katika shairi hilo
huku wakinukuu.
(ii) Waelekeze wanafunzi kukusanya kazi zao. Sahihisha kazi zao
na toa mrejesho.
Majibu
Majibu ya shughuli ya 4.10 (a) yatatokana na uelewa wa mwanafunzi.
Katika shughuli hii, mwanafunzi atachambua mitazamo iliyomo katika
shairi alilopewa.
Shughuli ya 4.10(b)
Hatua za ufundishaji
(i) Waongoze wanafunzi kukaa katika jozi kuchambua shughuli
ya 4.10 (b) iliyomo kwenye Kitabu cha Mwanafunzi, kisha
wawasilishe kwa majadiliano zaidi. Rekebisha dosari pale
zinapojitokeza na toa mrejesho wa shughuli hiyo kwa wakati.
44 Kiongozi cha Mwalimu
Kidato cha Tano
23/06/2024 17:48
FASIHI YA KISWAHILI KIONGOZI CHA MWALIMU KIDATO CHA TANO.indd 44 23/06/2024 17:48
FASIHI YA KISWAHILI KIONGOZI CHA MWALIMU KIDATO CHA TANO.indd 44