Page 55 - Fasihi ya Kiswahili kwa Shule za Sekondari Kiongozi cha Mwalimu Kidato cha Tano
P. 55

Fasihi ya Kiswahili  Shule za Sekondari


           Shughuli ya 4.14(b)
           Hatua za ufundishaji

             (i)   Waongoze wanafunzi kukaa katika vikundi kujadiliana shughuli
                  ya  4.14(b) iliyomo  kwenye Kitabu  cha  Mwanafunzi,  kisha
           FOR ONLINE READING ONLY
                  wakusanye kazi zao. Sahihisha na toa mrejesho kwa wakati.
           Majibu

           Majibu ya shughuli ya 4.14(b) yatatokana na uelewa wa mwanafunzi.
           Katika shughuli hii, mwanafunzi atachambua na kuhusianisha mitazamo
           na matendo ya jamii kutoka kwenye tamthiliya teule mbili.


             Somo la 5:  Athari za kiimani na kimtazamo katika bongo fleva,
                        mashairi na tamthiliya  zinavyojidhihirisha katika
                        jamii


           Shughuli ya 4.15(a)

           Hatua za ufundishaji

             (i)   Waongoze  wanafunzi  kutumia  vyanzo vya mkondoni na
                  vinginevyo  kupakua  na  kusikiliza  au  kutazama nyimbo
                  mbalimbali    zinazohamasisha     mapambano     ya    maisha
                  zilizoimbwa  na wasanii wa kike kisha kukaa katika vikundi
                  kufanya  shughuli  ya 4.15(a) iliyomo  kwenye Kitabu  cha
                  Mwanafunzi. Kila mwanafunzi afanye kazi binafsi kwa kujibu
                  maswali yaliyotolewa.

             (ii)  Waelekeze  wanafunzi kukusanya kazi walizozifanya katika
                  vikundi vyao, sahihisha na toa mrejesho.
           Majibu

           Majibu ya shughuli ya 4.15(a) yatatokana na uelewa wa mwanafunzi.
           Katika shughuli hii, mwanafunzi atachambua  athari za kiimani  na
           mitazamo katika wimbo huo kwa kujibu maswali yaliyotolewa.


                 Kiongozi cha Mwalimu                                    49
                    Kidato cha Tano



                                                                            23/06/2024   17:48
     FASIHI YA KISWAHILI KIONGOZI  CHA MWALIMU KIDATO CHA TANO.indd   49    23/06/2024   17:48
     FASIHI YA KISWAHILI KIONGOZI  CHA MWALIMU KIDATO CHA TANO.indd   49
   50   51   52   53   54   55   56   57   58   59   60