Page 64 - Fasihi ya Kiswahili kwa Shule za Sekondari Kiongozi cha Mwalimu Kidato cha Tano
P. 64
Fasihi ya Kiswahili Shule za Sekondari
(iii) Waongoze wanafunzi kufanya uwasilishaji. Chagua vikundi
vichache ili kuwakilisha vingine. Katika uwasilishaji,
hakikisha kila mwanafunzi anashiriki kwa kutoa maoni au
kuuliza maswali ili kuendeleza majadala. Rekebisha dosari pale
FOR ONLINE READING ONLY
zitakazojitokeza.
(iv) Waelekeze wanafunzi kukusanya na kusahihisha kazi ya kila
mwanafunzi ili kuondoa dosari zinazojitokeza na toa mrejesho
kwa wanafunzi wote.
Majibu
(i) Majibu ya shughuli ya 5.4 (a) yatategemea uelewa wa
mwanafunzi na tamthiliya teule atakazozitumia katika
uchambuzi. Katika uchambuzi, mwanafunzi azingatie misingi
ya ujumi ili kuitumia kuhakiki mbinu za kiujumi kwenye
kipande cha tamthiliya.
Shughuli ya 5.4 (b)
Hatua za ufundishaji
(i) Waongoze wanafunzi kusoma tamthiliya mbili teule kama
inavyoelekezwa katika shughuli ya 5.4 (b) iliyomo kwenye
Kitabu cha Mwanafunzi.
(ii) Waongoze wanafunzi kuchambua mbinu zilizotumika kujenga
ujumi katika tamthiliya teule, kisha chagua wanafunzi wachache
wawasilishe kwa niaba ya wenzao. Ongoza mjadala kisha
rekebisha upungufu unaojitokeza.
Majibu
Majibu ya shughuli ya 5.4 (b) yatategemea uelewa wa mwanafunzi na
tamthiliya teule atakazozitumia mwanafunzi katika uchambuzi. Katika
uchambuzi, mwanafunzi azingatie mbinu za kiujumi zilizotumituka
katika tamtiliya hizo.
58 Kiongozi cha Mwalimu
Kidato cha Tano
23/06/2024 17:48
FASIHI YA KISWAHILI KIONGOZI CHA MWALIMU KIDATO CHA TANO.indd 58
FASIHI YA KISWAHILI KIONGOZI CHA MWALIMU KIDATO CHA TANO.indd 58 23/06/2024 17:48