Page 63 - Fasihi ya Kiswahili kwa Shule za Sekondari Kiongozi cha Mwalimu Kidato cha Tano
P. 63

Fasihi ya Kiswahili  Shule za Sekondari


           Majibu
           Majibu ya shughuli 5.3(a) yatategemeana na uelewa wa mwanafunzi.
           Mwanafunzi ajibu maswali baada ya kusoma na kuchambua jigambo
           hilo kwa kuongozwa na maswali yaliyotolewa.
           FOR ONLINE READING ONLY

           Shughuli ya 5.3(b)
           Hatua za ufundishaji

             (i)   Waongoze  wanafunzi  kufanya shughuli ya 5.3(b) iliyomo
                  kwenye Kitabu cha Mwanafunzi.

             (ii)  Waelekeze wanafunzi kutumia kifaa chochote cha TEHAMA
                  kupakua jigambo lolote, kisha kuchambua mbinu ambazo
                  mtunzi amezitumia kujenga ujumi katika jigambo hilo.

             (iii)  Sahihisha kazi ya kila mwanafunzi ili kuondoa dosari
                  zitakazojitokeza na toa mrejesho kwa wanafunzi wote.

           Majibu
           Majibu ya shughuli 5.3(b) yanaweza  kutegemeana  na uelewa  wa
           mwanafunzi. Majibu ya shughuli hii yajikite katika kuchambua mbinu
           za kiujumi zilizotumika katika jigambo atakalochambua.


           Shughuli ya 5.4(a)
           Hatua za ufundishaji

             (i)   Waongoze wanafunzi kufanya shughuli ya 5.4 (a) iliyomo
                  kwenye Kitabu cha Mwanafunzi.

             (ii)  Waelekeze wanafunzi kukaa katika jozi ili kusoma matini fupi
                  ya tamthiliya, kisha kujibu maswali. Hakikisha kila mwanafunzi
                  anashiriki kikamilifu  katika majadiliano.  Sikiliza  mjadala na
                  uliza maswali ili kupima ushiriki wa kila mwanafunzi.





                 Kiongozi cha Mwalimu                                    57
                    Kidato cha Tano



                                                                            23/06/2024   17:48
     FASIHI YA KISWAHILI KIONGOZI  CHA MWALIMU KIDATO CHA TANO.indd   57    23/06/2024   17:48
     FASIHI YA KISWAHILI KIONGOZI  CHA MWALIMU KIDATO CHA TANO.indd   57
   58   59   60   61   62   63   64   65   66   67   68