Page 7 - Jiografia_Mazingira
P. 7
Utangulizi
Kitabu cha Jiografia na Mazingira kimetayarishwa kwa kuzingatia
muhtasari wa somo la Jiografia na Mazingira elimu ya msingi Darasa
FOR ONLINE READING ONLY
la III - VI uliotolewa na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia
mwaka 2023. Baadhi ya maudhui ya kitabu hiki yamechukuliwa
kutoka katika vitabu vya Maarifa ya Jamii Darasa la Tatu, la Nne
na la Tano vilivyochapishwa mwaka 2018 kwa kuzingatia muhtasari
wa mwaka 2016. Kitabu hiki kina sura nne, ambazo ni Dhana ya
ramani, Pande Kuu za Dunia, Uchoraji wa ramani sahili na Matumizi
ya ramani. Kwa kujifunza maudhui ya kitabu hiki utakuza maarifa,
stadi na mwelekeo katika kuchora, kusoma na kutafsiri ramani.
Maudhui ya kitabu hiki yamewasilishwa kwa njia ya matini, kazi za
kufanya, michoro na ramani mbalimbali ili kukuwezesha kujenga
umahiri uliokusudiwa katika kila sura. Kila sura ina mazoezi ya
kutosha yatakayokuwezesha kupima uelewa wako kuhusu maudhui
husika. Hivyo, unashauriwa kufanya kazi na mazoezi yote yaliyopo
katika kitabu hiki pamoja na kazi zingine utakazopewa na mwalimu
ili kujenga umahiri uliokusudiwa.
Jifunze zaidi kupitia Maktaba Mtandao https://ol.tie.go.tz au ol.tie.
go.tz
Taasisi ya Elimu Tanzania
vi
31/10/2024 19:17
JIOGRAFIA NA MAZINGIRA DARASA LA 4.indd 6
JIOGRAFIA NA MAZINGIRA DARASA LA 4.indd 6 31/10/2024 19:17