Page 8 - Jiografia_Mazingira
P. 8
Sura
ya Dhana ya ramani
Kwanza
FOR ONLINE READING ONLY
Utangulizi
Mandhari ya uso wa dunia hutofautiana kutoka eneo moja kwenda
lingine. Katika hali ya kawaida ni vigumu kufahamu mandhari ya
mahali fulani pasipo kutembelea eneo husika. Ramani ni mwongozo
unaorahisisha ujifunzaji kuhusu eneo fulani linalopatikana katika
uso wa dunia bila kufika katika eneo husika. Katika sura hii,
utajifunza maana ya ramani, aina za ramani, vipengele muhimu
vya ramani, sifa za ramani, na umuhimu wa ramani. Umahiri
utakaoujenga utakuwezesha kufafanua aina za ramani katika
miktadha mbalimbali.
Fikiri
Mwonekano wa maeneo mbalimbali ya uso wa dunia
Maana ya ramani
Ramani ni mchoro unaowakilisha taarifa zilizopo katika uso wa dunia
kwa kutumia skeli maalumu. Ramani huchorwa katika karatasi,
kitambaa, kidijitali au eneo lolote bapa. Taarifa za kijiografia zinazoweza
kuwasilishwa katika ramani ni kama vile; milima, mabonde, mito,
barabara, majengo na taarifa zingine muhimu. Ramani husaidia
kuelewa jinsi maeneo yalivyo na namna ya kuyafikia.
1
31/10/2024 19:17
JIOGRAFIA NA MAZINGIRA DARASA LA 4.indd 1
JIOGRAFIA NA MAZINGIRA DARASA LA 4.indd 1 31/10/2024 19:17