Page 9 - Jiografia_Mazingira
P. 9
Zoezi la kwanza
1. Kwa nini tunahitaji ramani?
2. Eleza tofauti iliyopo kati ya picha na ramani.
FOR ONLINE READING ONLY
Aina za ramani
Vigezo mbalimbali hutumika kuainisha aina za ramani. Kigezo
kimojawapo ni kuangalia lengo la ramani husika. Kwa kutumia
kigezo hiki, kuna makundi makuu mawili ya ramani. Makundi hayo
ni: ramani za jumla na ramani za thematiki.
Ramani za jumla
Hizi ni ramani zinazotoa taarifa za jumla kuhusu eneo fulani. Ramani
hizi hazitoi taarifa moja pekee, bali hutoa taarifa mbalimbali za eneo
husika. Kwa mfano; barabara, mito, mipaka ya kiutawala, makazi ya
watu, milima na uoto. Ramani hizi humsaidia mtumiaji kuelewa taarifa
za msingi za mahali fulani, uhusiano wa vitu mbalimbali vilivyopo,
pamoja na kutambua uelekeo katika uso wa dunia. Hivyo, ramani
za jumla ni kama vile; ramani za topografia, ramani za kisiasa, na
ramani za barabara na reli.
Ramani za topografia
Ramani hizi huwakilisha mwonekano wa maumbo mbalimbali ya asili
na yaliyotengenezwa na binadamu yanavyoonekana katika uso wa
dunia. Pia, hutumia mistari ya kontua kuonesha tofauti za miinuko
katika eneo husika la ardhi. Mfano wa maumbo ya asili ni kama vile:
bahari, maziwa, mito, tambarare, mabonde, milima, na uoto. Mfano
wa maumbo yaliyotengenezwa na binadamu ni pamoja na majengo,
na barabara, kama inavyoonekana katika Kielelezo namba 1. Hivyo,
ramani hizi ni muhimu katika kupanga shughuli za aina mbalimbali
kama vile ujenzi, utalii, kilimo, viwanda, uvuvi na biashara.
2
31/10/2024 19:17
JIOGRAFIA NA MAZINGIRA DARASA LA 4.indd 2
JIOGRAFIA NA MAZINGIRA DARASA LA 4.indd 2 31/10/2024 19:17