Page 13 - Jiografia_Mazingira
P. 13
Zoezi la pili
1. Utatumia aina gani ya ramani kukuongoza kwenda mkoa
ambao haujawahi kufika?
2. Kwa nini ramani za kisiasa hubadilika baada ya muda?
FOR ONLINE READING ONLY
3. Iwapo unataka kupanda mlima, ni ramani gani utaitumia
kufahamu mwinuko wa mlima huo?
Ramani za thematiki
Hizi ni ramani zinazowasilisha mada au taarifa moja maalumu na
pekee. Ramani za thematiki zinaweza kuwa za aina mbalimbali
kulingana na mada inayowasilishwa. Kwa mfano, ramani za thematiki
zinaweza kuwasilisha aina ya udongo, uoto, mazao, idadi ya watu,
hali ya hewa na mipango mji.
Ramani ya idadi ya watu
Ramani hii inaonesha wingi au mtawanyiko wa watu katika eneo
fulani. Ramani za idadi ya watu zinatusaidia kuona maeneo yenye
watu wengi au wachache. Zinasaidia watu wanaopanga kuhusu
mahali pa kuweka vitu muhimu kama shule, hospitali, masoko, na
barabara. Kielelezo namba 4 kinaonesha ramani ya mtawanyiko
wa watu katika mkoa wa Tabora mwaka 2022.
6
31/10/2024 19:17
JIOGRAFIA NA MAZINGIRA DARASA LA 4.indd 6
JIOGRAFIA NA MAZINGIRA DARASA LA 4.indd 6 31/10/2024 19:17