Page 18 - Jiografia_Mazingira
P. 18
Vipengele muhimu vya ramani
Vipengele muhimu vya ramani ni sehemu za msingi za ramani
zinazowezesha matumizi ya ramani husika. Maana na uhalisia wa
ramani umebebwa na sehemu hii muhimu. Vipengele hivi hufanya
FOR ONLINE READING ONLY
ramani ieleweke na yenye kuwasilisha taarifa za eneo husika kwa
usahihi. Vifuatavyo ni vipengele muhimu vinavyotakiwa kuzingatiwa
katika ramani:
(a) Fremu: ni mpaka au mstari wa nje unaozunguka ramani. Fremu
inasaidia kuweka wazi mipaka ya ramani na kuitenganisha na
taarifa nyingine kwenye ukurasa. Inaonesha ramani inapoanzia
na inapoishia;
(b) Kichwa cha ramani: Husaidia kuitambulisha ramani kwa
msomaji kuwa ramani inahusu nini au inawasilisha taarifa au
jambo gani la kijiografia. Kwa mfano, kama ramani inaonesha
barabara za Tanzania, kichwa cha ramani kinaweza kuwa
”Ramani ya barabara za Tanzania”;
(c) Uelekeo wa Kaskazini: Huonesha uelekeo katika ramani ambao
kwa kawaida huwasilishwa na alama ya ncha ya Kaskazini.
Alama hii inamwezesha msomaji kubaini pande zingine za dunia
katika ramani kama vile; Kusini, Mashariki na Magharibi. Kujua
uelekeo katika ramani kunakusaidia kuelewa mahali vitu vilipo
kwenye ramani;
(d) Ufunguo: Unafafanua ishara na alama zilizotumika katika
ramani. Kwa mfano, alama ya mti inaweza kuwakilisha msitu; na
mstari wa mawimbi wenye rangi ya bluu unaweza kuwakilisha
mto;
(e) Skeli: Inaonesha uhusiano wa umbali uliotumika katika ramani
na umbali halisi katika ardhi. Kwa mfano, Sentimeta moja
kwenye ramani inaweza kuwakilisha Kilometa kumi katika ardhi;
11
31/10/2024 19:17
JIOGRAFIA NA MAZINGIRA DARASA LA 4.indd 11
JIOGRAFIA NA MAZINGIRA DARASA LA 4.indd 11 31/10/2024 19:17