Page 22 - Jiografia_Mazingira
P. 22
(f) kusaidia wakati wa dharura, kama vile majanga ya moto na
mafuriko kwa kusaidia timu za uokoaji kubaini njia bora za
kufika eneo la tukio;
(g) kusaidia kujifunza kuhusu hali ya hewa katika maeneo mbalimbali
kwa kuonesha mtawanyiko wa mvua, uoto na shughuli za
FOR ONLINE READING ONLY
binadamu zinazofanyika;
(h) kuonesha mahali ambapo rasilimali muhimu za nchi zinapatikana.
Kwa mfano, mito, maziwa, misitu na madini;
(i) kuonesha makazi na idadi ya watu katika maeneo tofauti;
(j) kujua mipaka ya kiutawala, kama vile mipaka ya kimataifa,
mikoa, wilaya, na vijiji;
(k) kuonesha vivutio vya utalii kama vile Mlima Kilimanjaro, Bonde
la Ngorongoro, na hifadhi za wanyamapori. Hii husaidia kuvutia
watalii kutembelea maeneo haya; na
(l) kusaidia kuelewa historia ya mahali kwa kuonesha jinsi
palivyobadilika baada ya muda.
Zoezi la nne
1. Eleza jinsi ramani zinavyosaidia kukuza shughuli za utalii.
2. Mkulima anawezaje kutumia ramani?
Zoezi la marudio
Sehemu A: Chagua herufi ya jibu sahihi
1. Ramani ni nini?
(a) Uwakilishwaji wa vitu vilivyomo kwenye uso wa dunia kwa
kutumia uelekeo wa kaskazini.
(b) Uwakilishwaji wa vitu vilivyomo kwenye uso wa dunia kwa
kutumia skeli.
(c) Uwakilishwaji wa vitu vilivyomo kwenye uso wa dunia kwa
kutumia ufunguo.
15
31/10/2024 19:18
JIOGRAFIA NA MAZINGIRA DARASA LA 4.indd 15
JIOGRAFIA NA MAZINGIRA DARASA LA 4.indd 15 31/10/2024 19:18