Page 21 - Jiografia_Mazingira
P. 21
Sifa za ramani
Ramani nzuri inapaswa kuwa na sifa zifuatazo:
(a) Isomeke na kutafsiriwa kwa urahisi;
(b) ioneshe vipengele vyote muhimu vya ramani, kama vile skeli,
FOR ONLINE READING ONLY
fremu, chanzo, ufunguo, mistari ya gridi, kichwa cha ramani
na uelekeo wa Kaskazini;
(c) iwakilishe maeneo na umbali halisi, pamoja na kuweka vitu
kwa usahihi;
(d) itumie rangi na maandishi yanayoonekana ili kusaidia watumiaji
kuelewa vizuri;
(e) ioneshe taarifa pekee zinazohitajika kwa madhumuni husika;
(f) itumie alama, rangi na mitindo inayofanana kwenye ramani
yote ili ieleweke kwa urahisi; na
(g) iwe na taarifa za hivi karibuni ili kuhakikisha kila kitu kinachooneshwa
ni sahihi.
Umuhimu wa ramani
Ramani ni kama kitabu cha mwongozo wa dunia kinachotusaidia
kujifunza kwa kuchunguza na kuelewa sehemu zinazotuzunguka.
Hivyo, ramani ni zana muhimu sana ambayo hutumiwa na watu
katika miktadha mbalimbali. Zifuatazo ni baadhi ya sababu muhimu
za kutumia ramani.
(a) Kujifunza kuhusu maeneo mbalimbali, hata kama hatujawahi
kufika;
(b) kufahamu umbali kutoka sehemu moja hadi nyingine;
(c) kufahamu uelekeo wa kufuata ili kufika tulikokusudia, kama
Kaskazini, Kusini, Mashariki, au Magharibi;
(d) kupanga safari zetu kwa kubaini barabara bora, njia za mkato
na maeneo ya kuvutia tunayoweza kuyaona njiani;
(e) kuyafahamu mazingira yetu na vitu vilivyomo, kama vile milima,
mito, maziwa na misitu;
14
31/10/2024 19:18
JIOGRAFIA NA MAZINGIRA DARASA LA 4.indd 14 31/10/2024 19:18
JIOGRAFIA NA MAZINGIRA DARASA LA 4.indd 14