Page 26 - Jiografia_Mazingira
P. 26
Sura
ya Pande Kuu za Dunia
Pili
FOR ONLINE READING ONLY
Utangulizi
Binadamu anapotembea hufuata uelekeo fulani wa dunia ili
kufika sehemu aliyokusudia. Ili kubaini uelekeo sahihi, Pande
Kuu za Dunia hutumika. Kijiografia yapo majina maalumu
ambayo hutumika kubainisha Pande Kuu za Dunia. Katika sura
hii utajifunza kuhusu maana ya Pande Kuu za Dunia, kuchora,
na kubaini Pande Kuu za Dunia. Pia, utajifunza kuhusu pande
nane za dunia na umuhimu wa kutumia Pande Kuu za Dunia.
Umahiri utakaoujenga utakuwezesha kutumia Pande Kuu na
pande nane za Dunia kubaini mahali na uelekeo.
Fikiri
Namna ya kubaini njia kwa kutumia Pande Kuu za
Dunia
Maana ya Pande Kuu za Dunia
Pande Kuu za Dunia ni alama za msingi za mwongozo zinazotumika
kuonesha uelekeo wa sehemu tofauti za dunia. Uelekeo huo ni Kaskazini,
Kusini, Mashariki na Magharibi. Kila uelekeo unawakilisha upande
fulani wa dunia. Mara nyingi, Pande Kuu za Dunia zinapoandikwa
huwakilishwa kwa herufi. Kwa mfano, Kaskazini huwakilishwa
na herufi (Kas), Kusini huwakilishwa na herufi (Kus), Mashariki
huwakilishwa na herufi (Mas), na Magharibi huwakilishwa na herufi
(Magh). Alama za Pande Kuu za Dunia mara nyingi huoneshwa
19
31/10/2024 19:18
JIOGRAFIA NA MAZINGIRA DARASA LA 4.indd 19
JIOGRAFIA NA MAZINGIRA DARASA LA 4.indd 19 31/10/2024 19:18