Page 30 - Jiografia_Mazingira
P. 30
FOR ONLINE READING ONLY
Kielelezo namba 2: Kubaini Pande Kuu za Dunia kwa kutumia uelekeo wa kivuli
Kumbuka, ni vigumu kufanya utambuzi wa Pande Kuu za Dunia kwa
njia ya uelekeo wa kivuli wakati wa jua la utosi (saa sita mchana),
kwani katika muda huu kivuli chako kinakuwa kimekuzunguka.
Kazi ya kufanya namba 2
1. Nenda nje ya darasa wakati wa asubuhi, na simama eneo la
katikati ya shule yako;
2. Baini upande wa jua linakochomoza, kisha bainisha Pande
Kuu za Dunia na utaje vitu vinavyopatikana katika upande
husika.
3. Tengeneza kifani cha Pande Kuu za Dunia kwa kutumia
makunzi yanayopatikana katika mazingira uliyopo.
Zoezi la pili
Jibu maswali yafuatayo:
1. Ni uelekeo gani upo nyuma yako unapotazama upande wa
Kaskazini?
23
31/10/2024 19:18
JIOGRAFIA NA MAZINGIRA DARASA LA 4.indd 23 31/10/2024 19:18
JIOGRAFIA NA MAZINGIRA DARASA LA 4.indd 23