Page 29 - Jiografia_Mazingira
P. 29
Njia za kubaini Pande Kuu za Dunia
Pande Kuu za Dunia zinaweza kubainishwa kwa kutumia njia
mbalimbali. Njia hizi ni kwa kutumia mawio na machweo ya Jua,
uelekeo wa kivuli, uelekeo wa nyota, kwa kutumia ramani, na kwa
kutumia dira. Katika hatua hii tutajifunza kubaini Pande Kuu za
FOR ONLINE READING ONLY
Dunia kwa kutumia mawio na machweo ya Jua, uelekeo wa kivuli,
ramani, na dira.
Kubaini Pande Kuu za Dunia kwa kutumia mawio na machweo
ya Jua
Kuangalia Jua linapochomoza wakati wa asubuhi au linapozama
wakati wa jioni ni njia mojawapo ya kubaini Pande Kuu za Dunia
katika eneo ulilopo. Kwa kawaida, Jua huchomoza upande wa
Mashariki na kuzama upande wa Magharibi. Kitendo hiki cha asili
hurahisisha kutambua upande wa Mashariki na Magharibi wa mahali
ulipo. Kwa kutambua uelekeo wa mawio na machweo, unaweza
kukuza uelewa wa msingi wa Pande Kuu za Dunia.
Hivyo, wakati wa asubuhi, ukisimama kwa kulitazama Jua upande
huo ni Mashariki, na Magharibi ni upande ulikoelekeza mgongo.
Upande wa kulia utakuwa ni Kusini na upande wa kushoto ni
Kaskazini. Vivyohivyo, wakati wa jioni ukilitazama jua linapozama
upande huo ni Magharibi, wakati nyuma yako kutakuwa ni Mashariki,
kulia kwako ni Kaskazini na kushoto kwako ni Kusini.
Kubaini Pande Kuu za Dunia kwa kutumia uelekeo wa kivuli
Uelekeo wa kivuli chako wakati wa asubuhi na jioni unaweza kutumika
kubaini Pande Kuu za Dunia. Kwa kawaida, unapotembea wakati
wa asubuhi upande ambao kivuli chako kilipo ndio Magharibi. Kwa
mfano, ukitembea kwa kulitaza Jua, kivuli chako kitakuwa nyuma
yako, na ikiwa utatembea kwa kuligeuzia Jua mgongo, kivuli chako
kitakuwa mbele yako, hivyo, upande huo ni Magharibi. Vilevile,
wakati wa jioni, upande ambao kivuli chako kilipo ndio Mashariki
yako, kama inavyoonekana katika Kielelezo namba 2.
22
31/10/2024 19:18
JIOGRAFIA NA MAZINGIRA DARASA LA 4.indd 22 31/10/2024 19:18
JIOGRAFIA NA MAZINGIRA DARASA LA 4.indd 22