Page 31 - Jiografia_Mazingira
P. 31
2. Mwalimu wako akiwa ametazama upande wa Kaskazini,
kushoto kwake kutakuwa ni upande gani?
3. Kama umepotea msituni na ukabaini Jua linazama upande
wako wa kulia, je, wewe utakuwa umetazama upande gani?
FOR ONLINE READING ONLY
4. Unapotembea wakati wa jioni, endapo kivuli chako kitakuwa
mbele yako, je utakuwa unaelekea upande gani?
Kubaini Pande Kuu za Dunia kwa kutumia ramani
Ramani ni mwongozo mmojawapo unaotumika kubaini Pande Kuu
za Dunia. Miongoni mwa vipengele muhimu vya ramani ni alama
ya uelekeo wa Kaskazini. Matumizi ya alama hii katika ramani ni
kurahisisha kubaini Pande Kuu za Dunia yaani: Kaskazini, Kusini,
Mashariki na Magharibi.
Kazi ya kufanya namba 3
Chunguza Kielelezo namba 3 kisha; bainisha uelekeo wa
vitu kulingana na maelekezo uliyopewa;
Kielelezo namba 3: Mtaa wa ziwani
24
31/10/2024 19:18
JIOGRAFIA NA MAZINGIRA DARASA LA 4.indd 24
JIOGRAFIA NA MAZINGIRA DARASA LA 4.indd 24 31/10/2024 19:18