Page 32 - Jiografia_Mazingira
P. 32
Maswali
(a) Bainisha uelekeo wa kituo cha bajaji kwa kutokea eneo la
kambi.
(b) Fikiri, upo eneo yalipo makazi na unataka kwenda kivukoni,
FOR ONLINE READING ONLY
je, utafuata uelekeo gani?
(c) Ziwa lipo upande gani wa makazi?
(d) Kanisa lipo upande gani wa eneo la kambi?
(e) Msikiti upo upande gani wa viwanja vya michezo?
Kubaini Pande Kuu za Dunia kwa kutumia dira
Dira ni kifaa kinachotumiwa kutambua uelekeo wa Kaskazini. Zipo
aina mbili za dira, ambazo ni; dira ya kidijitali na dira ya analojia.
Dira ya kidijitali hutumia teknolojia kusoma na kuonesha uelekeo
wa Kaskazini. Aina hii ya dira imeunganishwa kwenye GPS, saa
za kisasa, simujanja na vyombo vya usafiri kama vile magari, boti
na ndege kama inavyoonekana katika Kielelezo namba 4. Dira ya
analojia hutumia vipande vya sumaku au sindano yenye sumaku
kuelekeza upande wa Kaskazini.
Kielelezo namba 4: Dira ya kidijitali
25
31/10/2024 19:18
JIOGRAFIA NA MAZINGIRA DARASA LA 4.indd 25
JIOGRAFIA NA MAZINGIRA DARASA LA 4.indd 25 31/10/2024 19:18