Page 33 - Jiografia_Mazingira
P. 33
Hatua za kubaini pande za dunia kwa kutumia dira
(a) Chukua dira yako au pakua programu tumizi ya dira;
(b) bofya programu tumizi ya dira na hakikisha mshale wa dira yako
umeelekea upande wa Kaskazini (Kas);
FOR ONLINE READING ONLY
(c) wakati mshale wa dira umeelekea upande wa Kaskazini, geuka
kuelekea upande huo. Hii itasaidia kutambua uelekeo wa Kaskazini
kwa kujua ni upande gani ambao mshale wa dira unaelekeza; na
(d) mara baada ya kutambua uelekeo wa Kaskazini, unaweza
kubaini pande nyingine za dunia. Kwa mfano, upande wa Kusini
utakuwa nyuma yako, Mashariki utakuwa upande wako wa kulia
na Magharibi utakuwa upande wako wa kushoto.
Kazi ya kufanya namba 4
Tumia simujanja, tabuleti au kompyuta. kupakua programu
tumizi ya dira, kisha baini Pande Kuu za Dunia katika
mazingira uliyopo.
Pande nane za dunia
Pande nane za dunia hutoa mielekeo minne zaidi ya Pande Kuu
za Dunia. Mielekeo hiyo ni Kaskazini-Mashariki (Kas-Mas), Kusini-
Mashariki (Kus-Mas), Kusini-Magharibi (Kus-Magh), na Kaskazini-
Magharibi (Kas-Magh). Pande hizi hutoa maelekezo ya kina au
uelekeo mahususi na sahihi zaidi kuhusu mahali. Kwa kawaida,
hutumiwa katika nyanja mbalimbali kama vile: katika usafiri wa anga
au majini, jiografia na utabiri wa hali ya hewa.
Hatua za kuchora pande nane za dunia;
(a) Chora Pande Kuu za Dunia kuonesha upande wa Kaskazini,
Kusini, Mashariki, na Magharibi;
(b) chora mstari ulionyooka katikati ya upande wa Kaskazini na
upande wa Mashariki, ukianzia pale mistari ya pande hizo
ilipokutana, kisha andika Kaskazini-Mashariki (Kas-Mas);
26
31/10/2024 19:18
JIOGRAFIA NA MAZINGIRA DARASA LA 4.indd 26
JIOGRAFIA NA MAZINGIRA DARASA LA 4.indd 26 31/10/2024 19:18