Page 34 - Jiografia_Mazingira
P. 34
(c) chora mstari mwingine ulionyooka katikati ya upande wa Kusini
na upande wa Mashariki, ukianzia pale mistari ya pande hizo
ilipokutana, kisha andika Kusini-Mashariki ( Kus-Mas);
(d) chora mstari mwingine ulionyooka katikati ya upande wa Kusini
na upande wa Magharibi, ukianzia pale mistari ya pande hizo
FOR ONLINE READING ONLY
ilipokutana kisha andika Kusini-Magharibi (Kus-Magh); na
(e) chora mstari mwingine ulionyooka katikati ya upande wa Kaskazini
na upande wa Magharibi, ukianzia pale mistari ya pande hizo
ilipokutana, kisha andika Kaskazini-Magharibi (Kas-Magh).
Baada ya kuchora mchoro wako, bila shaka umepata pande nane
za dunia.
Zingatia: Unaposoma au unapoonesha pande nane za dunia, unapaswa
kuanzia upande wa Kaskazini au Kusini. Hii ni kwa sababu pande
hizi ni alama za msingi katika dira zinazotumika katika uelekezaji.
Pia, alama hizi ndio msingi wa kukuongoza kutambua pande nane
za dunia, kama inavyoonekana katika Kielelezo namba 5.
Kielelezo namba 5: Pande nane za dunia
27
31/10/2024 19:18
JIOGRAFIA NA MAZINGIRA DARASA LA 4.indd 27 31/10/2024 19:18
JIOGRAFIA NA MAZINGIRA DARASA LA 4.indd 27