Page 36 - Jiografia_Mazingira
P. 36
(g) Sakina anaenda hotelini
(h) Sakina anaenda zahanati
Zoezi la tatu
FOR ONLINE READING ONLY
Jibu maswali yafuatayo:
1. Eleza tofauti kati ya Pande Kuu za Dunia na pande nane
za dunia.
2. Kwa nini tunapobainisha pande nane za dunia tunaanza
kusoma upande wa Kaskazini au Kusini?
3. Ni uelekeo gani upo katikati ya Kusini na Mashariki?
4. Endapo shule yako ipo Kaskazini-Magharibi mwa shule ya
rafiki yako, je, shule ya rafiki yako itakuwa upande gani?
Umuhimu wa Pande Kuu za Dunia
Pande Kuu za Dunia ni muhimu sana katika maisha yetu ya kila
siku. Ufuatao ni umuhimu wa kutumia Pande Kuu za Dunia;
(a) Husaidia kubaini uelekeo na mahali katika ramani na uso wa
dunia. Hii inawarahisishia watumiaji kutambua mahali walipo
na wanapokwenda; na kuweza kuwaelekeza watu namna ya
kufika mahali fulani kiurahisi.
(b) huwasaidia wahandisi na wasanifu majengo katika kufanya
ubunifu wa majengo, barabara na reli. Uelewa kuhusu Pande
Kuu za Dunia husaidia katika kubaini uelekeo wa eneo la
ujenzi kulingana na vigezo mbalimbali kama vile uelekeo wa
mawio na machweo ya Jua. Pia, husaidia kubaini uelekeo wa
barabara na reli kutoka sehemu moja kwenda sehemu nyingine.
(c) husaidia katika kuongoza vyombo vya usafiri. Pande Kuu za
Dunia humsaidia rubani, dereva au nahodha kuchagua njia
fupi na salama; na
29
31/10/2024 19:18
JIOGRAFIA NA MAZINGIRA DARASA LA 4.indd 29
JIOGRAFIA NA MAZINGIRA DARASA LA 4.indd 29 31/10/2024 19:18