Page 40 - Jiografia_Mazingira
P. 40
Sura Uchoraji wa ramani
ya sahili
Tatu
FOR ONLINE READING ONLY
Utangulizi
Ramani ni njia mojawapo inayotumika kuwasilisha taarifa za vitu
mbalimbali vinavyopatikana katika uso wa dunia. Katika sura
hii, utajifunza dhana ya uchoraji wa ramani, vitu vinavyoweza
kuoneshwa katika ramani, na alama za ramani. Pia, utajifunza
kuhusu skeli ya ramani, vifaa vya kuchorea ramani, hatua za
uchoraji wa ramani sahili, na uchoraji ramani kidijitali. Vilevile,
utajifunza kuchora ramani ya darasa, shule, kata, wilaya na
Tanzania. Umahiri utakaoujenga utakuwezesha kuchora ramani
sahili ya mazingira uliyopo.
Fikiri
Vitu vilivyopo katika uso wa dunia vinavyoweza
kuwakilishwa katika ramani
Dhana ya uchoraji wa ramani
Uchoraji wa ramani ni sanaa na sayansi ya kuonesha kwenye karatasi
au uso bapa wowote mahali ambapo vitu vinapatikana katika uso
wa dunia. Taaluma ya uchoraji wa ramani huitwa katografia, na mtu
anayechora ramani huitwa katografa. Katika uchoraji wa ramani,
tunatumia alama kuonesha vitu kama vile: barabara, nyumba, mito
na milima. Uchoraji huu huzingatia uwiano sahihi kati ya eneo, vitu
halisi na alama zitakazowekwa katika ramani.
Vitu vinavyoweza kuoneshwa katika ramani
Ramani hutumika kuonesha vitu mbalimbali kulingana na dhumuni
33
31/10/2024 19:18
JIOGRAFIA NA MAZINGIRA DARASA LA 4.indd 33
JIOGRAFIA NA MAZINGIRA DARASA LA 4.indd 33 31/10/2024 19:18