Page 41 - Jiografia_Mazingira
P. 41
lililokusudiwa. Kwa mfano, kupitia ramani, tunaweza kuona barabara
zinazoelekea sehemu mbalimbali, majengo kama nyumba na
shule, na mito na bahari kuonesha maeneo ya maji. Pia, tunaweza
kuona milima na mabonde kuonesha sehemu ya ardhi iliyoinuka
na kudidimia. Vilevile, huonesha maeneo ya kijani kama mbuga na
FOR ONLINE READING ONLY
misitu, mipaka ya miji na nchi, na viwanja vya michezo.
Hata hivyo, sio kila kitu kilichopo katika uso wa dunia huoneshwa
kwenye ramani. Vitu vinavyooneshwa kwenye ramani ni vile ambavyo
ni muhimu kwa watumiaji wa ramani hiyo. Maamuzi ya nini kinapaswa
kuwekwa katika ramani yanafanywa na mchoraji wa ramani kwa
kuzingatia mahitaji ya watumiaji wa ramani husika. Hivyo, ramani
huonesha vitu muhimu pekee vilivyokusudiwa kuwasilishwa ili
kuifanya isomeke na kueleweka kwa urahisi.
Kazi ya kufanya namba 1
Tembelea maeneo kuzunguka shule yako, kisha orodhesha
vitu muhimu ambavyo ungevionesha iwapo ungetakiwa kuchora
ramani ya shule.
Alama za ramani
Ramani haiwezi kuonesha vitu kama vilivyo katika uhalisia wake.
Hivyo, hutumia alama mahususi za ramani. Alama za ramani ni
michoro midogo inayotumika kwenye ramani kuwakilisha vitu halisi.
Unapotaka kuonesha vitu halisi katika ramani, unapaswa kutumia
alama za vitu hivyo. Alama hizi husaidia kuelezea vitu hivyo kwa
njia rahisi na inayoeleweka vizuri. Pia, alama za ramani huoneshwa
kwenye ufunguo wa ramani. Ufunguo wa ramani hutumika kufafanua
alama zote zilizotumika kwenye ramani. Kielelezo namba 1 kinaonesha
baadhi ya alama zinazotumika katika ramani.
34
31/10/2024 19:18
JIOGRAFIA NA MAZINGIRA DARASA LA 4.indd 34 31/10/2024 19:18
JIOGRAFIA NA MAZINGIRA DARASA LA 4.indd 34