Page 46 - Jiografia_Mazingira
P. 46
(d) weka alama ya uelekeo wa Kaskazini upande wa juu kulia mwa
ramani kuonesha uelekeo ya Kaskazini, Kusini, Mashariki na
Magharibi;
(e) chora umbo linalowakilisha mipaka ya eneo unalotaka kulionesha
kwenye ramani ndani ya mstatili au mraba uliochora hapo awali;
FOR ONLINE READING ONLY
(f) tumia alama kuchora vitu muhimu katika uelekeo sahihi ndani
ya umbo la mipaka ya eneo; ulilochora. Anza na vitu vikubwa
kisha umalizie na vitu vidogo;
(g) andaa ufunguo unaofafanua alama zote zilizotumika kwenye
ramani;
(h) andika kichwa cha ramani sahili;
(i) hakikisha ramani inaonesha vitu vyote muhimu, na fanya
marekebisho panapohitajika; na
(j) chora mraba au mstatili (fremu) kuzunguka ramani na vitu vyote
muhimu vya ramani.
Kuchora ramani sahili ya darasa
Zifuatazo ni hatua za kufuata ili kuchora ramani ya darasa kuonesha
vitu vilivyopo kama vile: meza na kiti cha mwalimu, meza na viti au
madawati ya wanafunzi, mlango, madirisha na vitu vingine muhimu.
(a) Tambua ukubwa, umbo na uelekeo wa darasa;
(b) bainisha maumbo, ukubwa na mahali vitu muhimu vilipo darasani;
(c) andaa eneo litakalotumika kuchora ramani ya darasa, kwa kuchora
umbo la mraba au mstatili kwenye karatasi. Hakikisha umeacha
eneo kwa ajili ya kichwa cha ramani, ufunguo na maelezo; na
(d) fuata hatua za uchoraji wa ramani sahili kuchora ramani ya
darasa.
Kazi ya kufanya namba 3
Fuata hatua za uchoraji wa ramani sahili, kuchora ramani
ya darasa lako ukionesha vitu vyote muhimu vilivyomo darasani.
39
31/10/2024 19:18
JIOGRAFIA NA MAZINGIRA DARASA LA 4.indd 39 31/10/2024 19:18
JIOGRAFIA NA MAZINGIRA DARASA LA 4.indd 39