Page 50 - Jiografia_Mazingira
P. 50
Maswali
1. Chagua wilaya moja, kisha chora ramani yake kwenye
daftari lako;
2. Katika ramani ya wilaya uliyochora, onesha vitu vifuatavyo:
FOR ONLINE READING ONLY
(a) Makao makuu ya wilaya;
(b) Msitu;
(c) Soko; na
(d) Hospitali ya wilaya.
Kazi ya kufanya namba 7
Tumia Atlasi au vyanzo vya kuaminika vya mtandaoni
kupata ramani ya Tanzania inayoonesha mipaka ya
kiutawala, kisha baini mkoa unaoishi na fanya yafuatayo:
(a) Chora ramani ya mkoa unaoishi;
(b) Onesha wilaya za mkoa huo;
(c) Weka kivuli kwenye wilaya unayoishi;
(d) Weka alama ya ncha ya Kaskazini kuonesha uelekeo; na
(e) Weka ufunguo wa ramani.
Kuchora ramani ya Tanzania
Ramani ya Tanzania inatoa taarifa mbalimbali kuhusu nchi ya Tanzania.
Taarifa zinazooneshwa katika ramani ya Tanzania zinatofautiana
kulingana na dhumuni la ramani hiyo. Kwa mfano, ramani ya Tanzania
inaweza kuonesha mahali mji mkuu ulipo, Mlima Kilimanjaro, reli,
bahari, maziwa, mipaka ya mikoa na ya nchi jirani.
43
31/10/2024 19:18
JIOGRAFIA NA MAZINGIRA DARASA LA 4.indd 43
JIOGRAFIA NA MAZINGIRA DARASA LA 4.indd 43 31/10/2024 19:18