Page 52 - Jiografia_Mazingira
P. 52
Mambo ya kuzingatia
Uchoraji wa ramani kidijitali kwa kutumia programu ya “Google My
Maps” unazingatia mambo yafuatayo;
(a) Uwepo wa simujanja, tabuleti au kompyuta;
FOR ONLINE READING ONLY
(b) hakikisha kifaa kimeunganishwa na mtandao;
(c) tambua eneo la kijiografia unalotaka kuchora katika ramani,
mfano mipaka ya nchi, barabara au ziwa; na
(d) hakikisha una akaunti katika tovuti ya Google kwa kujisajili
kwanza. Tumia anuani ya “Google My Maps” katika kujisajili.
Anuani hii itakuruhusu kuunda ramani mwenyewe kwa kuchora
maumbo na kuweka alama za vitu mbalimbali.
Hatua za uchoraji wa ramani kwa kutumia programu ya ‘Google
My Maps’
Zifuatazo ni hatua za kufuata unapochora ramani kwa kutumia
programu ya “Google My Maps.” Ramani ya hifadhi ya Wanyama
ya Swaga Swaga iliyopo mkoa wa Dodoma imetumika kama mfano.
1. Tumia kivinjari chako, ingia katika tovuti ya ‘Google’ kisha andika
‘Google My Maps’ kama inavyoonekana katika Kielelezo namba
7, kisha bofya sehemu imeandikwa “My Maps”
Kielelezo namba. 7: Kivinjari cha wavuti
45
31/10/2024 19:18
JIOGRAFIA NA MAZINGIRA DARASA LA 4.indd 45
JIOGRAFIA NA MAZINGIRA DARASA LA 4.indd 45 31/10/2024 19:18