Page 54 - Jiografia_Mazingira
P. 54
FOR ONLINE READING ONLY
Kielelezo namba 10: Ikoni mbalimbali zinazoweza kutumika katika uchoraji
ramani
5. Anza kuchora ramani kwa kufuatilia mipaka ya hifadhi ya Swaga
Swaga kama inavyoonekana katika Kielelezo namba 11.
Kielelezo namba 11: Uchoraji wa mpaka wa hifadhi ya Swaga Swaga
6. Endelea kuchora hadi utakapokamilisha mzunguko wa eneo
la hifadhi ya Swaga Swaga. Ukimaliza mzunguko, kishale cha
kipanya kitabadilika kutoka alama ya kujumlisha kwenda alama
ya kidole. Bofya kitufe cha kushoto cha kipanya au bofya mara
mbili kitufe cha kulia cha kipanya cha kompyuta kukamilisha
uchoraji. Mwisho, andika neno Swaga Swaga kwenye neno
“polygon 1” na bofya neno “save” kama inavyoonekana kwenye
Kielelezo namba 12.
47
31/10/2024 19:18
JIOGRAFIA NA MAZINGIRA DARASA LA 4.indd 47
JIOGRAFIA NA MAZINGIRA DARASA LA 4.indd 47 31/10/2024 19:18