Page 56 - Jiografia_Mazingira
P. 56
9. Kuweka ufunguo wa ramani bofya vidoti vitatu vya chini (1)
upande wa kushoto wa ramani, chagua “Rename this layer”
(2), andika neno ufunguo kwenye boksi la “Edit layer name” (3),
kisha bofya kitufe cha “Save” (4), kama inavyoonekana katika
Kielelezo namba 14.
FOR ONLINE READING ONLY
Kielelezo namba 14: Kuweka ufunguo wa ramani ya eneo ulilolichora
10. Chapisha ramani yako kwa ajili ya matumizi ya baadae. Ramani
ya kidijitali inaweza kuchapishwa kwa njia mbili. Njia ya kwanza
ni kuchapisha kama faili la PDF na njia ya pili ni kuchapisha
kama picha. Ili kuweza kufanya hivyo, nenda kwenye vidoti vitatu
(1), kisha chagua neno “Print map” (2), kama inavyoonekana
katika Kielelezo namba 15.
Kielelezo namba 15: Kuchapisha ramani
49
31/10/2024 19:18
JIOGRAFIA NA MAZINGIRA DARASA LA 4.indd 49
JIOGRAFIA NA MAZINGIRA DARASA LA 4.indd 49 31/10/2024 19:18