Page 53 - Jiografia_Mazingira
P. 53
2. Ingia katika menyu ya unda ramani mpya (create new maps)
kwenye “Google My Maps” kama inavyoonekana katika Kielelezo
namba 8.
FOR ONLINE READING ONLY
Kielelezo namba 8: Menyu ya kuunda ramani katika programu ya ‘Google
My Maps’
3. Tafuta anuani ya sehemu unayoihitaji katika ramani kama vile
majina ya mbuga, hifadhi, vijiji, kata, wilaya au mikoa. Kwa mfano,
andika “Swaga Swaga Game Reserve,” kama inavyoonekana
kwenye Kielelezo namba 9.
Kielelzo namba 9: Kiolesura cha programu ya “Google My Maps” kwa ajili
ya kutafuta eneo la kijiografia
4. Bofya alama ya kutafuta (search) ili kuonesha eneo la hifadhi ya
Swaga Swaga kama inavyoonekana katika Kielelezo namba 10.
Baada ya eneo la hifadhi ya Swaga Swaga kuonekana unaweza
kuanza kuchora mipaka yake. Kuanza kuchora mipaka ya
Swaga Swaga, bofya ‘draw line’ (1) kisha ‘Add line or shapes’
(2) kama inavyoonekana katika Kielelezo namba 10.
46
31/10/2024 19:18
JIOGRAFIA NA MAZINGIRA DARASA LA 4.indd 46
JIOGRAFIA NA MAZINGIRA DARASA LA 4.indd 46 31/10/2024 19:18