Page 58 - Jiografia_Mazingira
P. 58
Zoezi la marudio
Chagua herufi ya jibu sahihi
1. Skeli 1:100 000 inaweza kuwasilishwa kwa njia ya maneno kama
ifuatavyo:
FOR ONLINE READING ONLY
(a) Sentimeta moja kwenye ramani inawakilisha Kilometa miamoja
kwenye ardhi.
(b) Kilometa moja kwenye ramani inawakilisha Sentimeta laki
moja kwenye ardhi.
(c) Sentimeta moja kwenye ramani inawakilisha Sentimeta laki
moja kwenye ardhi.
(d) Sentimeta miamoja elfu kwenye ramani inawakilisha Sentimeta
moja kwenye ardhi.
2. Ni programu gani ya kidijitali iliyotumika kuchora ramani ya hifadhi
ya Swaga Swaga katika sura ya tatu?
(a) “ArcGIS”
(b) “QGIS”
(c) “AutoCAD”
(d) “Google My Maps”
3. Kitufe kipi kinatumika kuchora barabara katika ramani za kidijitali?
(a) ’Add direction’.
(b) ’Add line or shape’.
(c) ’Add marker’.
(d) ’Draw polygon’.
4. Taaluma ya uchoraji wa ramani hujulikana kama______________.
(a) uchoraji wa ramani
(b) ubunifu wa ramani
(c) katografia
(d) katografa
51
31/10/2024 19:18
JIOGRAFIA NA MAZINGIRA DARASA LA 4.indd 51
JIOGRAFIA NA MAZINGIRA DARASA LA 4.indd 51 31/10/2024 19:18