Page 59 - Jiografia_Mazingira
P. 59
5. Rangi gani kati ya zifuatazo huwakilisha uoto?
(a) Nyeusi
(b) Kijani
(c) Rangi ya giza
FOR ONLINE READING ONLY
(d) Ugoro
6. Eleza ni kwa namna gani ramani inaweza kuwakilisha eneo
kubwa la ardhi.
7. Eleza hatua za kufuata unapochora ramani sahili.
8. Chora ramani ya kata yako kwa njia ya kidijitali.
9. Chora alama za ramani zinazowakilisha vitu vifuatavyo:
(a) Reli;
(b) njia ya waenda kwa miguu;
(c) shule; na
(d) mlima.
10. Chora ramani sahili ya nyumbani kwenu ukibainisha vitu vilivyopo
Kaskazini, Kusini, Mashariki na Magaharibi mwa nyumba.
Msamiati
Kiolesura Sura ya programu fulani katika kompyuta
Kipanya Kifaa cha kompyuta chenye vitufe viwili vya kubofya
kulia na kushoto, kinachofanya kazi kwa kutumia alama
ya mshale au kiganja, kung’amua na kufungua taarifa
mbalimbali ndani ya kompyuta.
Kivinjari Programu tumizi inayomuwezesha mtumiaji kusoma
na kuunganishwa na taarifa zingine zilizomo ndani ya
wavuti kuu.
Wavuti Mtandao wa mawasiliano ya kompyuta wenye taarifa
mbalimbali za kimataifa.
52
31/10/2024 19:18
JIOGRAFIA NA MAZINGIRA DARASA LA 4.indd 52 31/10/2024 19:18
JIOGRAFIA NA MAZINGIRA DARASA LA 4.indd 52