Page 64 - Jiografia_Mazingira
P. 64
Maswali
1. Jengo gani liko karibu zaidi na ziwa?
2. Baini jengo lililo karibu zaidi na zahanati.
3. Jengo gani liko karibu na ofisi?
FOR ONLINE READING ONLY
4. Ni majengo gani mengine yapo karibu na ziwa?
5. Baini jengo lililo mbali zaidi na uwanja wa mpira wa miguu.
Kupitia ramani, unaweza kubaini umbali kutoka sehemu moja hadi
nyingine kwa kufuata hatua zifuatazo;
(a) Kupima umbali kwenye ramani kutoka sehemu moja hadi
nyingine; na
(b) Kubadili umbali wa kwenye ramani kuwa umbali halisi wa
kwenye ardhi kwa kutumia skeli.
Upimaji huu unahusisha vitu vilivyonyooka na visivyonyooka. Upimaji
huu unaweza kufanyika katika ramani za kidijitali na zisizo za kidijitali.
Upimaji wa umbali ulionyooka
Umbali ulionyooka katika ramani hupimwa kwa kutumia kipande
cha karatasi, uzi, rula, bikari na skeli. Katika sehemu hii utatumia
kipande cha karatasi, rula na skeli.
1. Kwa kutumia kipande cha karatasi
Hatua zifuatazo hutumika kupima umbali katika ramani kwa kutumia
kipande cha karatasi na skeli:
(a) Chora mstari ulionyooka unaounganisha vituo viwili ulivyopewa
katika ramani, kwa mfano, kituo A na B kama inavyoonekana
katika Kilelezo namba 4
A B
Kielelezo namba 4: Mstari ulionyooka unaounganisha kituo A na B
57
31/10/2024 19:18
JIOGRAFIA NA MAZINGIRA DARASA LA 4.indd 57
JIOGRAFIA NA MAZINGIRA DARASA LA 4.indd 57 31/10/2024 19:18