Page 62 - Jiografia_Mazingira
P. 62
kwenye uso wa dunia. Pia, itakuwezesha kubaini uelekeo wa kutoka
sehemu moja hadi nyingine.
Vilevile, tunaweza kubaini uelekeo na mahali kwa kutumia ramani za
kidijitali na GPS. GPS hutumika kubaini mahali ulipo, wakati ramani
ya kidijitali huonesha sehemu mbalimbali pamoja na pale unapotaka
FOR ONLINE READING ONLY
kwenda. Baada ya kubaini mahali ulipo na unakokwenda, GPS
hukokotoa na kuonesha umbali na uelekeo wa kufuata. Ramani za
kidijitali na GPS zinapatikana katika vifaa vya kielektroniki kama vile,
simujanja, tabuleti na kompyuta. Makundi mbalimbali ya watu kama
vile, manahodha, madereva, marubani, wanajiolojia na masorovea
hutumia ramani katika kazi zao ili kubaini mahali, umbali na uelekeo.
Kazi ya kufanya namba 2
Chunguza Kielelezo namba 2, kisha jibu maswali
yanayofuata kwa kutumia alama ya uelekeo wa Kaskazini.
Ramani sahili ya Mtaa wa Songambele
Katherin David
Barabara ya uzunguni Barabara ya warioba
Mahakama Maktaba
Barabara ya maktaba Soko
Juma
Barabara ya majengo
Mwajuma
Barabara ya muungano
Hawa Shule ya msingi
Jose Festo
Songambele
Ufunguo
Bustani Nyumba Soko
Barabara Taasisi
Kielelezo namba 2: Mtaa wa Songambele
GSPublisherVersion 0.12.100.100
55
31/10/2024 19:18
JIOGRAFIA NA MAZINGIRA DARASA LA 4.indd 55 31/10/2024 19:18
JIOGRAFIA NA MAZINGIRA DARASA LA 4.indd 55