Page 61 - Jiografia_Mazingira
P. 61
Kutumia ramani kubaini uelekeo na mahali
Kazi ya kufanya namba 1
Chunguza Kielelezo namba 1, kisha jibu maswali yanayofuata:
FOR ONLINE READING ONLY
Kielelezo namba 1: Ramani ya shule
Maswali
1. Ni vitu gani vinapatikana Kaskazini mwa barabara kuu?
2. Madarasa yako upande gani wa uwanja wa mpira wa miguu?
3. Darasa la VI linapatikana upande gani wa Darasa la V?
4. Darasa la II linapatikana upande gani wa Darasa la IV?
5. Upande gani wa eneo la shule ambao hauna uzio?
Uelekeo na mahali katika ramani unaweza kubainishwa kwa kutumia
alama ya uelekeo wa Kaskazini. Alama ya uelekeo wa Kaskazini
itakuonesha ni upande upi wa ramani upo Kaskazini, Kusini, Mashariki
au Magharibi. Hii itakuwezesha kubaini mahali vilipo vitu mbalimbali
54
31/10/2024 19:18
JIOGRAFIA NA MAZINGIRA DARASA LA 4.indd 54
JIOGRAFIA NA MAZINGIRA DARASA LA 4.indd 54 31/10/2024 19:18