Page 60 - Jiografia_Mazingira
P. 60
Sura
ya Matumizi ya ramani
Nne
FOR ONLINE READING ONLY
Utangulizi
Katika maisha, mara nyingi inatulazimu kusafiri kutoka sehemu
moja kwenda sehemu nyingine tusiyoifahamu kufuata huduma,
kupumzika au kutembelea ndugu na marafiki. Kunaweza kuwa
na ugumu fulani kuifikia sehemu husika pale unapokosa mtu
wa kukuongoza. Hata hivyo, ramani ni zana mojawapo muhimu
inayoweza kusaidia kubaini njia na kukuongoza kufika au
kufahamu kuhusu mahali husika. Katika sura hii, utajifunza
namna ya kutumia ramani kubaini uelekeo, umbali, mipaka
ya kiutawala na sura ya nchi. Pia, utajifunza kutumia ramani
kubaini mtawanyiko wa vitu na watu katika eneo fulani. Umahiri
utakaoujenga utakuwezesha kutumia ramani katika miktadha
mbalimbali.
Fikiri
Unavyoweza kufika sehemu usiyoifahamu
kwa kutumia ramani
53
31/10/2024 19:18
JIOGRAFIA NA MAZINGIRA DARASA LA 4.indd 53
JIOGRAFIA NA MAZINGIRA DARASA LA 4.indd 53 31/10/2024 19:18