Page 55 - Jiografia_Mazingira
P. 55
FOR ONLINE READING ONLY
Kielelezo namba 12: Umbo lililokamilika la ramani ya hifadhi ya Swaga
Swaga
7. Unaweza kubadilisha kichwa cha habari kulingana na maudhui
ya ramani. Mfano tumia ramani ya hifadhi ya Swaga Swaga.
Nenda kwenye dirisha la kushoto mwa ramani, chagua “untitled
map” kisha andika “Ramani ya Swaga Swaga” kwenye boksi
lililoandikwa “Map title” na bofya kitufe cha “Save”.
8. Badili mwonekano wa ramani yako kwa kutumia rangi mbalimbali
zinazopatikana. Bofya kitufe cha kushoto cha kipanya ndani ya
hifadhi ya Swaga Swaga, kisha bofya tena kitufe cha “Style”
chagua rangi uipendayo, kwa mfano rangi ya kijani kama
inavyoonekana katika Kielelezo namba 13.
Kielelezo namba 13: Kubadilisha rangi katika ramani
48
31/10/2024 19:18
JIOGRAFIA NA MAZINGIRA DARASA LA 4.indd 48
JIOGRAFIA NA MAZINGIRA DARASA LA 4.indd 48 31/10/2024 19:18