Page 51 - Jiografia_Mazingira
P. 51
Kazi ya kufanya namba 8
1 Tumia atlasi au vyanzo vya kuaminika vya mtandaoni,
tafuta ramani ya Tanzania, kisha uichore na kuonesha vitu
vifuatavyo:
FOR ONLINE READING ONLY
(a) Mlima Kilimanjaro;
(b) Bahari ya Hindi;
(c) Ziwa Victoria;
(d) Ziwa Tanganyika;
(e) Ziwa Nyasa; na
(f) Visiwa vya Pemba, Unguja na Mafia.
2 Weka ufunguo, alama ya uelekeo wa Kaskazini, fremu na
kichwa cha ramani katika ramani uliyoichora.
Zoezi la tatu
1 Kujua kuchora ramani ya Tanzania kuna faida gani?
2 Katika ramani ya Tanzania, ni vitu gani muhimu vinapatikana
kwenye mipaka ya Tanzania na nchi jirani?
Uchoraji wa ramani kidijitali
Uchoraji wa ramani kidijitali ni uundaji wa ramani kwa kutumia
teknolojia ya kompyuta au Simujanja zenye programu za uchoraji
ramani kama vile; ‘ArcGIS’, ‘QGIS’, ‘AutoCAD’ na ‘Google My Maps’.
Kila programu ina sifa zake katika uchoraji wa ramani.
Katika ngazi hii, utajifunza uchoraji ramani za kidijitali kwa kutumia
programu ya “Google My Maps”. Uchoraji wa ramani kwa kutumia
programu ya “Google My Maps” ni rahisi kwa kutumia wavuti au
programu tumizi za simujanja. “Google My Maps” ina kiolesura
kinachomruhusu mtumiaji/mchoraji kutumia kompyuta kwa urahisi
na kuchora ramani kwa haraka bila kuhitaji utaalamu mkubwa.
44
31/10/2024 19:18
JIOGRAFIA NA MAZINGIRA DARASA LA 4.indd 44
JIOGRAFIA NA MAZINGIRA DARASA LA 4.indd 44 31/10/2024 19:18