Page 47 - Jiografia_Mazingira
P. 47
Kuchora ramani sahili ya shule
Ramani ya shule ni mchoro unaoonesha muundo wa shule, kama vile
viwanja vya michezo, majengo yakiwemo; vyumba vya madarasa,
ofisi za waalimu, na maeneo mengine muhimu. Hatua zifuatazo
zitakuwezesha kuchora ramani ya shule:
FOR ONLINE READING ONLY
(a) Tambua ukubwa, umbo na uelekeo wa eneo la shule;
(b) bainisha ukubwa, maumbo na mahali vilipo vitu muhimu katika
eneo la shule;
(c) andaa eneo litakalotumika kuchora ramani ya shule, kwa kuchora
umbo la mraba au mstatili kwenye karatasi. Hakikisha umeacha
eneo kwa ajili ya kichwa cha ramani, ufunguo na maelezo; na
(d) fuata hatua za uchoraji wa ramani sahili kuchora ramani ya
shule.
Kazi ya kufanya namba 4
Chora ramani sahili kuonesha mazingira ya shule yako
kwa kuzingatia hatua za uchoraji wa ramani ya shule.
Zoezi la pili
1. Ni vifaa gani muhimu unapaswa kuviandaa unapotaka
kuchora ramani?
2. Chora alama zinazotumika kuwakilisha vitu vifuatavyo:
(a) Majengo;
(b) miti;
(c) barabara;
(d) msikiti;
(e) kanisa; na
(f) daraja.
3. Eleza tofauti ya ramani ya darasa na ramani ya shule.
4. Eleza kazi ya ufunguo katika ramani.
40
31/10/2024 19:18
JIOGRAFIA NA MAZINGIRA DARASA LA 4.indd 40
JIOGRAFIA NA MAZINGIRA DARASA LA 4.indd 40 31/10/2024 19:18