Page 45 - Jiografia_Mazingira
P. 45
FOR ONLINE READING ONLY
Rula Penseli Bikari
Kalamu ya
Kiguni Ufutio wino
Kielelezo namba 4: Baadhi ya vifaa vya uchoraji wa ramani
Vifaa vingine vinavyoweza kutumika katika uchoraji wa ramani ni
kama kompyuta, simujanja, tabuleti, ubao wa kuchorea wa kidijitali
na kalamu ya kuchorea ya kidijitali. Pia, mchoraji anaweza kuhitaji
programu za kuchorea kama vile: programu za “Computer Aided
Design” (CAD) na “Geographical Information System” (GIS).
Kuchora ramani sahili
Ramani sahili huchorwa bila kutumia skeli kuonesha mahali vitu
vinapopatikana kwenye uso wa dunia.
Hatua za uchoraji wa ramani sahili
(a) Ili kuchora ramani sahili, ni vema kutambua ukubwa, umbo na
uelekeo wa eneo unalotaka kulionesha kwenye ramani sahili;
(b) bainisha maumbo, ukubwa na mahali vitu muhimu vinapopatikana
katika eneo unalotaka kulionesha kwenye ramani;
(c) andaa eneo litakalotumika kuchora ramani sahili, kwa kuchora
umbo la mraba au mstatili kwenye karatasi. Hakikisha umeacha
eneo kwa ajili ya kichwa cha ramani, ufunguo na maelezo;
38
31/10/2024 19:18
JIOGRAFIA NA MAZINGIRA DARASA LA 4.indd 38 31/10/2024 19:18
JIOGRAFIA NA MAZINGIRA DARASA LA 4.indd 38