Page 44 - Jiografia_Mazingira
P. 44
Skeli ya ramani
Skeli ya ramani ni uwiano wa umbali kwenye ramani na umbali halisi
kwenye ardhi. Skeli ya ramani husaidia kuonesha namna vipimo vya
ramani vinavyolingana na vipimo halisi. Skeli inaweza kuwasilishwa
kwa njia ya maelezo, uwiano au sehemu, na mstari.
FOR ONLINE READING ONLY
Njia ya maelezo
Skeli ya maelezo huonesha uwiano wa umbali kwenye ramani
na umbali halisi kwenye ardhi kwa kutumia maneno. Kwa mfano,
“Sentimeta moja kwenye ramani inawakilisha Kilometa moja kwenye
ardhi”.
Njia ya uwiano au sehemu
Skeli ya uwiano au sehemu huonesha uwiano kati ya umbali kwenye
ramani na umbali halisi kwenye ardhi kwa kutumia namba. Kwa
1
mfano, 1:50000 au 50000 .
Njia ya mstari
Skeli ya mstari huonesha uwakilishi wa kijiografia wa umbali wa ardhi
kwa kutumia mstari. Kielelezo namba 3 kinaonesha skeli ya mstari.
1000 500 1
Meta 0 1 2 3 Kilometa
Kielelezo namba 3: Skeli ya mstari
Vifaa vya kuchorea ramani
Kuna vifaa mbalimbali vinavyotumika katika uchoraji wa ramani. Vifaa
GSPublisherVersion 0.12.100.100
hivyo ni pamoja na meza ya kuchorea, karatasi, kalamu ya risasi
(penseli), bikari, kiguni, ufutio, kalamu ya wino, kichongeo, rangi za
kuchorea na rula kama inavyoonekana katika Kielelezo namba 4.
37
31/10/2024 19:18
JIOGRAFIA NA MAZINGIRA DARASA LA 4.indd 37 31/10/2024 19:18
JIOGRAFIA NA MAZINGIRA DARASA LA 4.indd 37