Page 65 - Jiografia_Mazingira
P. 65
(b) Chukua kipande cha karatasi, kunja kupata ukingo ulionyooka.
Laza ukingo huo sambamba na mstari AB na uweke kwa usahihi
na kuandika alama kufuata mstari AB. Hakikisha unalingana
kabisa na alama A na B kama inavyoonekana katika Kielelezo
namba 5.
FOR ONLINE READING ONLY
A B
A Karatasi iliyokunjwa B
Kielelezo namba 5: Kupima umbali kutoka kituo A hadi B kwa kutumia kipande
cha karatasi
(c) Umbali kutoka kituo A hadi B kwenye kipande cha karatasi
unaweza kubadilishwa kuwa umbali halisi kwenye ardhi kwa
kutumia skeli ya mstari au skeli ya uwiano. Kwa kutumia skeli
ya mstari kipande cha karatasi huwekwa sambamba na skeli
ya mstari kwa kuoanisha kituo A na sifuri (0) na kituo B upande
wa kulia wa skeli ya mstari. Iwapo kituo B kitaoana na namba
fulani kwenye skeli kama inavyoonekana kwenye kielelezo
namba 6, namba hiyo huwakilisha umbali halisi kwenye ardhi
kutoka kituo A hadi B. Kwahiyo, umbali wa kwenye ardhi kutoka
kituo A hadi B ni kilometa 3
1000 500
Meta 0 1 2 3 Kilometa
A Karatasi iliyokunjwa B
Kielelezo namba 6: Kituo B kimeoana na namba 3 inayowakilisha umbali wa
kilometa 3 kutoka kituo A hadi B
58
31/10/2024 19:18
JIOGRAFIA NA MAZINGIRA DARASA LA 4.indd 58
JIOGRAFIA NA MAZINGIRA DARASA LA 4.indd 58 31/10/2024 19:18