Page 67 - Jiografia_Mazingira
P. 67
(d) Kwa kutumia skeli ya uwiano, tumia rula kupima umbali wa
kwenye ramani kutoka kituo A hadi kituo B kwenye kipande
cha karatasi. Kwa mfano, iwapo umbali wa ramani kati ya kituo
A na B ni Sentimeta 5 na skeli ya uwiano ni 1:50000, umbali
halisi kwenye ardhi kutoka kituo A hadi B unaweza kupatikana
FOR ONLINE READING ONLY
kwa kufanya yafuatayo;
Umbali halisi kwenye ardhi (Km) = Umbali kwenye ramani (Sm) x
Namba ya chini kwenye skeli ya uwiano
= Sentimeta 5 x Sentimeta 50000
= Sentimeta 250000
Ikiwa kilometa 1 = sentimeta 100000, umbali halisi kwenye ardhi
unaweza kubadilishwa kutoka sentimeta kwenda kilometa kama
ifuatavyo:
Umbali kwenye ardhi (Km) =
Umbalikwenye ardhikatika Sentimeta
d Sentimeta100000 n # Kilo meta 1
= Sentimeta 250000 X Kilometa 1
Sentimeta 100000
= Kilometa 2.5
Kwa hiyo, umbali kwenye ardhi ni kilometa 2.5
60
31/10/2024 19:18
JIOGRAFIA NA MAZINGIRA DARASA LA 4.indd 60
JIOGRAFIA NA MAZINGIRA DARASA LA 4.indd 60 31/10/2024 19:18