Page 69 - Jiografia_Mazingira
P. 69
(a) Chora mstari ulionyooka unaounganisha vituo viwili, kwa mfano,
kituo A na kituo B kama inavyoonekana katika Kielelezo namba
9.
A B
FOR ONLINE READING ONLY
Kielelezo namba 9: Mstari ulionyooka unaounganisha kituo A na kiuo B
(b) Laza rula sambamba na mstari ulionyooka, hakikisha alama
ya sifuri (0) kwenye rula inashabihiana na kituo A (1), na weka
alama kwenye rula katika kituo B kama ilivyoonekana kwa
alama nyekundu (2) katika Kielelezo namba10.
B
A
(2)
(1)
Kielezo namba 10: Kupima umbali ulionyooka kwa kutumia rula
(c) Umbali katika ramani uliopimwa kwa rula kati ya kituo A hadi
B unaweza kubadilishwa kuwa umbali halisi katika ardhi kwa
kutumia skeli ya mstari au skeli ya uwakilishi wa sehemu
(uwiano) kwa kufuata hatua zifuatazo.
GSPublisherVersion 0.5.100.100
(i) Laza rula kwenye skeli ya mstari ambapo sifuri (0) ya
kwenye rula iwe sambamba na sifuri (0) ya kwenye skeli
ya mstari, na alama nyekundu iwe upande wa kulia wa
skeli ya mstari;
62
JIOGRAFIA NA MAZINGIRA DARASA LA 4.indd 62 31/10/2024 19:19
31/10/2024 19:19
JIOGRAFIA NA MAZINGIRA DARASA LA 4.indd 62