Page 73 - Jiografia_Mazingira
P. 73
pale kilipoishia kituo B kama inavyoonekana katika Kielelezo
namba 14.
FOR ONLINE READING ONLY
Kielelezo namba 14: Kufuatisha mstari kwa uzi kutoka kituo A hadi kituo B
(c) Tumia skeli ya mstari kubadili umbali wa kwenye ramani
kwenda umbali halisi kwenye ardhi kwa kufanya yafuatayo;
(i) Nyoosha uzi na ulaze katika skeli ya mstari, hakikisha
fundo la kwanza linalala kwenye sifuri (0) na fundo la pili
upande wa kulia wa skeli ya mstari;
(ii) Ikiwa fundo la pili lipo sambamba na namba fulani kwenye
skeli ya mstari, namba hiyo inawakilisha umbali halisi katika
ardhi kati ya vituo viwili;
(iii) Ikiwa fundo la pili liko katikati ya namba mbili, nakili
namba ya kushoto na weka alama nyekundu kwenye uzi
kama inavyoonekana katika Kielelezo namba 15. Kwa
mfano, namba ya kushoto iliyonakiliwa kwenye Kielelezo
namba 15 ni Km 1. Kisha, hamisha uzi kwenda kushoto
hadi kufikia fundo la pili liwe sambamba na sifuri (0) na
alama nyekundu iliyowekwa iwe upande wa kushoto wa
skeli ya mstari;
(iv) Mwisho, nakili namba iliyopo kwenye skeli ya mstari pale
ilipoishia alama nyekundu ya kwenye uzi. Kwa mfano, meta
500 imenakiliwa kama inavyoonekana katika Kielelezo
namba 15. Hivyo, umbali wa ardhi kati ya pointi A na B ni
Kilometa 1 na meta 500.
66
31/10/2024 19:19
JIOGRAFIA NA MAZINGIRA DARASA LA 4.indd 66 31/10/2024 19:19
JIOGRAFIA NA MAZINGIRA DARASA LA 4.indd 66