Page 77 - Jiografia_Mazingira
P. 77
Maswali
1. Tumia uzi kukokotoa umbali wa kutoka Kilimani hadi Hekima.
2. Tumia kipande cha karatasi kukokotoa urefu wa reli.
FOR ONLINE READING ONLY
3. Tumia bikari kukokotoa urefu wa mto Bariadi kutoka katika
kilele cha mlima hadi Ziwa Gagadi.
Kupima umbali kidijitali
Pamoja na kubaini umbali wa vitu vilivyonyooka na visivyonyooka
kwa kutumia njia za kawaida, pia tunaweza kubaini umbali kwenye
ramani kwa kutumia njia za kidijitali. Hatua zifuatazo zinaeleza
namna ya kutumia programu ya “Google My Maps” kupima umbali:
(a) Tumia kompyuta au simujanja kufungua tovuti ya Google,
kisha tafuta “Google My Maps” na bofya “My Maps” kama
inavyoonekana kwenye Kielelezo namba 21.
Kielelezo namba 21: Kufungua programu ya Google My Maps
(b) Baada ya kufungua “Google My Maps”, tafuta eneo unalotaka
kupima umbali kati ya vituo viwili. Kwa mfano, tutatafuta
Munguri FDC kama inavyoonekana kwenye Kilelezo namba
22 ili kupima umbali kati ya Munguri FDC na shule ya msingi
Munguri.
70
31/10/2024 19:19
JIOGRAFIA NA MAZINGIRA DARASA LA 4.indd 70
JIOGRAFIA NA MAZINGIRA DARASA LA 4.indd 70 31/10/2024 19:19