Page 79 - Jiografia_Mazingira
P. 79
FOR ONLINE READING ONLY
(b)
Kielelezo namba 23: Kuongeza ukubwa ili kuonesha njia inayounganisha
vituo viwili
(d) Ili kupima umbali, chagua alama ya rula kama inavyoonekana
kwenye Kielelezo namba 24. Alama hii inakuwezesha kupima
umbali wa vitu kama barabara, reli na mito, na pia kupima
maeneo ya vitu kama misitu, mabwawa, maziwa na mipaka
ya utawala.
Kielelezo namba 24: Kuchagua alama ya rula kwa ajili ya kupima umbali
(e) Kisha, sogeza kishale na bofya kwenye alama ya kwanza (yaani
Munguri FDC) (1) na anza kupima umbali kwa kufuata njia
kuelekea shule ya msingi Munguri (2), kama inavyoonekana
kwenye Kielelezo namba 25. Endelea kufuata njia hadi utafika
shule ya msingi Munguri. Ukifika shule ya msingi Munguri,
bofya mara mbili kumaliza kupima umbali na kuonesha umbali
72
31/10/2024 19:19
JIOGRAFIA NA MAZINGIRA DARASA LA 4.indd 72
JIOGRAFIA NA MAZINGIRA DARASA LA 4.indd 72 31/10/2024 19:19